29. Msimamo wa Sayyid Qutwub juu ya Mizani


Ninaapa kwa Allaah ya kwamba Sayyid Qutwub anapinga Mizani na anapinga Kuonekana kwa Allaah. Katika mambo mengi yuko pamoja na madhehebu ya Jahmiyyah na Mu´tazilah. Ninaapa kwa Allaah huu ndio uhakika wa mambo. Ninayasema haya ili watu wasije kudanganyika na vitabu vya mtu huyu. Ninaapa kwa Allaah vimejaa upotevu katika mambo ya misingi ya misingi mikubwa. Sayyid Qutwub alikuwa amechanganyikiwa na mpotevu. Vijana wengi watapotea kwa sababu ya kumtakasa na kumpandisha daraja zaidi na anavyostahiki. Hutopata Mu´taziliy au Jahmiy ambaye anazusha isipokuwa anashirikiana nao katika Bid´ah hiyo na kuweka hilo wazi kwa niaba yao. Inasikitisha sana. Anapinga Mizani, ´Arshi na mambo mengine mengi. Ni khatari.

Imaam Ahmad amesema:

“Inatakiwa kuamini Mizani siku ya Qiyaamah.”

Mu´tazilah, Jahmiyyah, Baatwiniyyah na wapotevu wengine wanapinga mambo haya.

Imaam Ahmad amesema:

“Yanatakiwa kuaminiwa na kuthibitishwa. Mwenye kurudisha hilo anatakiwa kupuuzwa na asijadiliwe.”

Hivi sasa tunajua jinsi ya kutaamiliana na mijadala.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 392
  • Imechapishwa: 26/08/2017