Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake ya kwamba Qadaatah amesema:

“Allaah ameumba nyota hizi kwa ajili ya mambo mtatu; mapambo ya mbingu, vimondo dhidi ya mashaytwaan na alama za kuongozwa njia. Yeyote atakayefasiri vinginevyo kakosea na kupoteza fungu lake na kajikalifisha kwa kitu asichokuwa na ujuzi nacho.”

2- Qadaatah amechukizwa kujifunza elimu ya vituo vya mwezi kama ambavyo Ibn ´Uyaynah pia hakuruhusu hilo. Hayo yamepokelewa na Harb kutoka kwa hao wawili. Ahmad na Ishaaq wameruhusu kujifunza elimu ya vituo vya mwezi.

3- Abu Muusa amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu sampuli tatu hawatoingia Peponi; chapombe, mwenye kukata udugu na mwenye kusadikisha uchawi.”[1]

Ameipokea Ahmad na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

MAELEZO

Mwandishi ametaja unajimu kwa sababu ni kitu kilichoenea. Unajimu ni kule kubahatisha tafaasiri za nyota. Unajimu unahusiana na kujulisha kutokana na hali za nyota yale yatayotendeka ardhini. Matokeo yake wanatazama nyota na namna zilivyokusanyika na zilivyoachana, kuzama kwake na kutua kwake, kuwa kwake karibu na kuwa kwake mbali. Kupitia mambo hayo wanajulisha kwamba ardhini kutatokea mambo kadhaa. Jambo hili ni la batili na ni katika kudai kujua mambo yaliyofichikana ambayo yamebatilishwa na Allaah pale aliposema:

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ

“Sema: “Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye yaliyofichikana isipokuwa Allaah na wala hawajui lini watafufuliwa.” (an-Naml 27:65)

Ama kutazama nyota kwa ajili ya kujua mashukio ya mwezi, nyakati za swalah na kujua ni wapi Qiblah kipo ni sawa na hakuna ubaya. Kama alivosema Ahmad na Ishaaq bin Raahuyah.

1- al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake ya kwamba Qadaatah amesema:

“Allaah ameumba nyota hizi kwa ajili ya mambo mtatu; mapambo ya mbingu, vimondo dhidi ya mashaytwaan na alama za kuongozwa njia. Yeyote atakayefasiri vinginevyo kakosea na kupoteza fungu lake na kajikalifisha kwa kitu asichokuwa na ujuzi nacho.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

لَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ

“Hakika Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mataa na tukazifanya kuwa ni makombora kwa mashaytwaan.” (al-Mulk 67:05)

وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ

“… na [zinawapeni] alama za kutambulisha – na kwa nyota [watu] wanaojiongoza njia.” (an-Nahl 16:16)

Qataadah amesema:

“Yeyote atakayefasiri vinginevyo kakosea na kupoteza fungu lake na kajikalifisha kwa kitu asichokuwa na ujuzi nacho.”

Bi maana mwenye kusema kuwa zinafahamisha jambo fulani katika mambo yaliyofichikana basi amekosea, amepoteza fungu lake na amezungumza asichokuwa nacho ujuzi. Maneno Yake:

وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ

“… na [zinawapeni] alama za kutambulisha – na kwa nyota [watu] wanaojiongoza njia.”

Hii ni elimu ya mashukio na upepo.

2- Qadaatah amechukizwa kujifunza elimu ya vituo vya mwezi kama ambavyo Ibn ´Uyaynah pia hakuruhusu hilo. Hayo yamepokelewa na Harb kutoka kwa hao wawili. Ahmad na Ishaaq wameruhusu kujifunza elimu ya vituo vya mwezi.

Haya ni maoni yasiyokuwa na nguvu. Ahmad na Ishaaq wote wawili wameliruhusu hilo na ndio maoni ya sawa.

3- Abu Muusa amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu sampuli tatu hawatoingia Peponi; chapombe, mwenye kukata udugu na mwenye kusadikisha uchawi.”

Kuhusu chapombe ameambiwa kwa minajili ya kumtishia kwa sababu ni dhambi kubwa. Chapombe anaingia katika utashi wa Allaah muda wa kuwa hajatubia. Lakini ikiwa anaonelea kuwa ni halali anakufuru. Kadhalika kukata udugu ni katika madhambi makubwa.

Ama kuhusu mwenye kuamini uchawi, ikiwa anaona kuwa uchawi ni haki na kwamba unayageuza mambo na kwamba mchawi yuko katika haki na kwamba anajua mambo yaliyofichikana, huyu ni kafiri. Ama ikiwa anaamini kuwa uchawi upo na kwamba una athari lakini pamoja na hivyo akakubali kuwa ni haramu na ni dhambi, huyu hakuna neno juu yake kwa sababu Allaah ameeleza kuhusu kuwepo kwa uchawi:

وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ

“Wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi.” (al-Baqarah 02:102)

[1] Ahmad (19587), Ibn Hibbaan (5346) na al-Haakim (7234). Nzuri kupitia zengine kwa mujibu wa Shu´ayb al-Arnaa’uut.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 18/10/2018