29. Mkusanyiko wa Badr ulikuwa bila miadi


Kutokana na hekima ya Allaah akawakusanya pasi na miadi yoyote. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ ۙ وَلَـٰكِن لِّيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا

“Lau mngeliahidiana basi mngelitofautiana katika miadi hiyo, lakini ili Allaah akidhie jambo lilokuwa lazima litendwe.”[1]

Pindi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipopata khabari kwamba Quraysh wametoka na wako njiani akawataka ushauri Maswahabah wake. Muhaajiruun wengi wakaongea na akawafanya vizuri. Kisha akawataka ushauri tena na huku akitaka kusikia vile wanavoonelea Answaar. Sa´d bin Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni kama kwamba unatulenga sisi. Ninaapa kwa Allaah, ee Mtume wa Allaah, ya kwamba lau utapasua bahari basi sisi tuko nyuma yako. Tuchukue, ee Mtume wa Allaah, kutokana na baraka za Allaah.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafurahishwa na hilo na akasema: ”Nendeni na pateni bishara! Kwani hakika Allaah ameniahidi moja katika makundi mawili.”

Baada ya hapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaenda na akatua maeneo karibu na Badr. Alipanda kipando (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yeye na mmoja katika Maswahabah wake  kwa ajili ya kupata khabari. Kisha akenda zake. Ilipofika jioni akamtuma ´Aliy, Sa´d na az-Zubayr kwenda Badr pwani ili kupeleleza khabari. Wakarudi na watumwa wawili wa Quraysh wakati ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amesimama yuko anaswali. Baadaye akawauliza: ”Nyinyi ni kina nani?” Wakajibu: ”Sisi ni watumisi wa Quraysh.”

[1]  08:42

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 47
  • Imechapishwa: 04/05/2018