29. Maneno ya Ashaa´irah juu ya Qur-aan yamefanana na maneno ya manaswara

Ashaa´irah wakaja kwa imani ya ajabu katika masuala haya; hawako pamoja na Jahmiyyah na wala hawako pamoja na Ahl-us-Sunnah. Wamesema kuwa maneno ni ile maana iliyosimama kwenye nafsi ya Mungu. Kuhusu Qur-aan hii na maneno yaliyoteremshwa kwa Mitume ni maelezo na simbulizi ya maneno ya Allaah. Kwa hiyo – yaani hiyo Qur-aan ambayo ni maana – imeumbwa. Kwa sababu Muhammad au Jibriyl wameelezea kuhusu maneno ya Allaah. Allaah hazungumzi. Maneno Yake ni maana iliyosimama kwenye nafsi Yake anayoyaelezea Mtume. Wamekusanya kati ya vinyume viwili ambavyo havikusemwa na mwengine zaidi yao. Matokeo yake wakafanya sehemu ya Qur-aan haikuumbwa, nayo ni ile maana ilioko kwenye nafsi, na matamshi yake yameumbwa. Qur-aan hii ilioko na sisi hii leo sio maneno ya Allaah. Ni maneno ya Muhammad au ya Jibriyl. Pia yameumbwa au Jibriyl ameyachukua kutoka katika Ubao uliohifadhiwa. Kwa hiyo sio maneno ya Allaah. Ni simbulizi au maelezo kuhusu maneno ya Allaah. Ashaa´irah ndio wanaosema kuwa ni maelezo. Maaturiydiyyah ndio wanaosema kuwa ni simbulizi. Wote wanaona kuwa sio maneno ya Allaah. Kwa sababu maneno ya Allaah ni maana iliyosimama kwenye nafsi peke yake. Sehemu ya Qur-aan ni ya kiungu na sehemu nyingine ni ya kimtu. Ni kama mfano wa maneno ya manaswara juu ya ´Iysaa ambao wanaona sehemu ya ´Iysaa ni ya Allaah na sehemu yake nyingine imeumbwa. Vivyo hivyo maneno ya Ashaa´irah yanafanana na maneno ya manaswara juu ya al-Masiyh. Wanaona kuwa baadhi yake imeumbwa na baadhi yake haikuumbwa. Migongano mitupu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 16/03/2021