Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Inatakiwa kuamini kuwa ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) atashuka na kumuua karibu na mlango wa Ludd.”

MAELEZO

Imepokelewa kwamba ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam) atateremka wakati ambapo waislamu wanasubiri Fajr. Atakuwa amevaa shuka mbili za juu za manjano na atakuwa ameweka mikono yake miwili juu ya mbawa za Malaika wawili. Wakati kutapokimiwa swalah al-Mahdiy atamwambia:

“Tangulia mbele, ee roho ya Allaah.” Aseme: “Maimamu wenu ni kutokamana na nyinyi.”

Kisha atoke kwenda kumtafuta ad-Dajjaal, mikononi mwake atakuwa na mkuki. Atamkuta karibu na mlango wa Ludd na atamuua hapo. Halafu atawaendea waumini awapongeze na awaeleze ngazi zao Peponi. Imepokelewa vilevile kwamba atamuuoa msichana wa al-Mahdiy ambaye atamfungulia njia.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 24/04/2019