Swali 29: Ni lini mtu anajizuilia siku ya ijumaa kugusa changarawe na kutumia Siwaak? Je, ni kuanzia pale ambapo imamu anapanda mimbari au ni pale Khutbah inapoanza? Mimi nawaona watu wengi hawajizuilii kutumia Siwaak isipokuwa pale ambapo imamu anaanza Khutbah na wengine wanaitumia katikati ya Khutbah. Tunamwomba muheshimiwa Shaykh atuelekeze katika usawa na Allaah akujaze kheri[1].

Jibu: Sunnah ni kuinyamazia Khutbah na kuacha kutumia Siwaak na vitu vyengine vya upuuzi tangu pale anapoianza mpaka pale anapoimaliza kwa ajili ya kutendea kazi Hadiyth ambazo ni Swahiyh zilizopokelewa katika hilo.

Lakini anayeingia msikitini na huku imamu anatoa Khutbah basi aswali swalah ya mamkuzi ya msikiti kabla ya kuketi chini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapofika mmoja wenu siku ya ijumaa na imamu anatoa Khutbah, basi arukuu Rak´ah mbili na azifupishe.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/336-337).

[2] al-Bukhaariy (1100) na Muslim (1449) na tamko ni lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 69
  • Imechapishwa: 01/12/2021