Namalizia kitabu hiki kwa kuwanukuu wanachuoni wetu wakubwa na wenye kuzingatiwa juu ya al-Albaaniy na walivomsifu. Katika hayo amesema muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allaah):

“Nimepokea barua yako na nimechoelewa ni kwamba unataka kuandika wasifu mpana kuhusu Shaykh na ´Allaamah Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Mnataka pia kujua vile ninavyomuonelea.

Naweza kukwambia kwamba Shaykh uliyemtaja anatambulika vyema kwetu juu ya kuwa na ´Aqiydah nzuri, mfumo na muendelezo wake wa kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) pamoja na juhudi zake kubwa katika kuzitumikia Hadiyth ambapo amezibainisha Hadiyth Swahiyh, dhaifu na zilizozuliwa na vitabu vyengine alivyoandika kwa undani kabisa juu ya maudhui hayo. Anatakiwa kushukuriwa juu ya yote hayo. Matendo yake yanawanufaisha waislamu. Namuomba Allaah amlipe maradufu, amsaidie aendelee kufanyakazi juu ya njia hii na kuifanya juhudi yake kuwa ni yenye furaha na mafanikio.”

Hivo ndivo alivosema Muftiy wa Saudi Arabia (Rahimahu Allaah) kumuhusu Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kwamba ni mtu aliye na ´Aqiydah na mfumo mzuri.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 05/12/2018


Takwimu
  • 25
  • 413
  • 1,821,444