29. Dalili juu ya mkono wa Allaah 15

29- Ahmad bin Muhammad bin Sulaymaan ametuhadithia: ´Umar bin Shabbah ametuhadithia: Abu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa ´Abdillaah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:

“Kuna mwanamume kutoka katika watu wa Kitabu alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Allaah (´Azza wa Jall) atazibeba mbingu kwenye kidole, milima na ardhi kwenye kidole, miti na maji kwenye kidole na viumbe kwenye kidole. Kisha aseme: “Mimi ndiye mfalme.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana. Kisha akasoma:

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria na hali ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Ametakasika na upungufu na yu juu kabisa kuliko yale wanayomshirikisha.”[1]

[1] 39:67

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 67-69
  • Imechapishwa: 28/02/2018