29. Aina ya sita ya majina ya haramu


6- Jina lisiloendana na yule mpewaji kwa sababu ima ni madai, kujitakasa au uongo ambalo halikubaliki kabisa. Mfano wa hayo ni yale yaliyotajwa katika Hadiyth iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Jina lenye kutwezwa zaidi kwa Allaah ni mtu mwenye kujiita “Mfalme wa wafalme”…. “

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Hali kadhalika majina kama hayo yaliyoharamishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama Mfalme wa wafalme, Hakimu wa mahakimu na Qaadhiy wa maqadhiy.

Humo kunaingia vilevile majina kama Bwana wa watu, Bwana wa wote, Bwana wa mabwana na bwana wa wanawake. Ni haramu pia mbali na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuitwa “Bwana wa wanaadamu”. Zaynab bint Abiy Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msizitakase nafsi zenu. Allaah ndiye anawajua wema zaidi katika nyinyi.”

Ameipokea Muslim.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 25
  • Imechapishwa: 18/03/2017