Kuna aina mbili ya uzazi wa mpango:

1- Kufunga kizazi milele. Haijuzu kwa sababu kunazuia mimba na kunapunguza kizazi. Kunaenda kinyume na malengo ya Shari´ah inayoamrisha kukithirisha Ummah wa Kiislamu. Hakuna kitu chenye kumpa dhamana kuwa mtoto wa mwanamke aliyepo hivi sasa hawezi kufa na akabaki hali ya kuwa hana mtoto.

2- Kupanga uzazi kwa muda. Kwa mfano mwanamke anapata ujauzito sana na hilo linamuudhi. Hivyo akataka kupangilia uzazi ili ashike mimba mara moja kwa kila miaka miwili na kadhalika. Inajuzu kwa sharti mume amkubalie na asidhurike kwa hilo. Dalili ya hilo ni kuwa Maswahabah walikuwa wakitumia mtindo wa al-´Azl, kuchopoa kabla ya kumwaga katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili wake zao wasipate mimba. Hawakukatazwa. al-´Azl ni mume kufanya jimaa na mke wake na pale anapotaka kumwaga akatoa uume wake na kumwaga nje ya uke.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016