28. Vipi mtu anatakiwa kupangusa akianza kupangusa akiwa mkazi kisha baadaye akasafiri?

Swali 28: Vipi mtu anatakiwa kupangusa akianza kupangusa akiwa mkazi kisha baadaye akasafiri?

Jibu: Akianza kupangusa hali ya kuwa ni mkazi kisha akasafiri, basi atatakiwa kukamilisha kupangusa hali ya kuwa ni msafiri kutokana kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu. Kuna wanazuoni waliosema kuwa akianza kupangusa katika hali ya ukazi kisha akasafiri basi atakamilisha akiwa ni mkazi. Lakini maoni yenye nguvu ni yale tuliyosema. Kwa sababu mtu huyu kumebaki kitu katika muda wa kupangusa kwake kabla ya kuanza safari. Kwa vile amesafiri anakuwa ni mwenye kuingia katika wasafiri wanaotakiwa kufuta michana mitatu na nyusiku zake. Imetajwa namna ambavo Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amechagua maoni haya baada ya kuonelea kwamba anatakiwa kukamilisha upungusaji hali ya kuwa ni mkazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/175)
  • Imechapishwa: 06/05/2021