28. Radd juu ya utata wa kwamba shirki ni kule kumili na kuitafuta sana dunia

Kumi na mbili: Wafuasi wanaofuata madhehebu ya Suufiyyah na wale vifaranga vyao wanadai kwamba shirki ni kule kumili kwenye dunia na kujishughulisha kuitafuta.

Jibu ni kwamba wanachokusudia kwa kusema hivi ni kuwa wanachotaka ni kufunika ile shirki kubwa waliyomo ikiwakilishwa na kuyaabudu makaburi na kupetuka mipaka kwa Mashaykh. Kutafuta dunia kwa njia iliyoruhusiwa ni miongoni mwa mambo yaliyoamrishwa na Allaah. Ikiwa malengo ya kuitafuta mtu anataka kumsaidie kumtii Allaah basi hiyo ni ´ibaadah na Tawhiyd.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 43
  • Imechapishwa: 03/04/2019