5- Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya haki ya mawalii na maimamu:

Maimamu wa Shari´ah hii ya Kiislamu ni wenye kutambulika na Ummah unatambua nafasi zao. Lakini hawaonelei kuwa wamekingwa na kukosea. Kwa mtazamo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawaoni yeyote kukingwa na kukosea wala kumkubalia kosa lake isipokuwa tu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amekingwa kukubaliwa kosa. Ama wengine vovyote atavofikia katika uimamu si mwenye kukingwa na kukosea kabisa. Kila mmoja anakosea, kila mmoja yanachukuliwa maneno yake na kuachwa isipokuwa tu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye tumeamrishwa na Allaah kumtii kwa njia isiyofungamana.

Wanaona kuwa hapana shaka kuwa katika Ummah huu kuna maimamu na mawalii. Lakini kwa kusema hivo hatukusudii kumthibitishia yeyote katika maimamu hawa kukingwa na kukosea, kumthibitishia yeyote katika mawalii ya kwamba anajua mambo yaliyofichikana au kwamba anaendesha ulimwengu. Hawamfanyi walii yule mwenye kujiita mwenyewe kwamba ni walii au akafanya propaganda batili ili kuwavuta watu kwake. Wanasema kuwa walii amebainishwa na Allaah pale aliposema:

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika – wale ambao wameamini na wakawa wanamcha Allaah.”[1]

Hawa ndio mawalii ambao wameamini na wakamcha Allaah. Imani ni ´Aqiydah. Kumcha Allaah ni matendo sawa ya kimaneno au kivitendo. Shaykh-ul-Islaam amechukua kutoka katika Aayah hii ibara nzuri isemayo:

“Yule ambaye ni muumini na mchaji Allaah ndiye walii wa Allaah.”

Huu ndiye walii wa kikweli. Walii sio yule ambaye anawavuta watu kwake na anakusanya watu na kuanza kutangaza kwamba anaweza kufanya na akawataka msaada mashaytwaan juu ya kujua yaliyojificha. Matokeo yake watu wakastaajabu kwa anayoyasema na kuanza kufikiria kuwa ni walii. Uwalii unakuwa kwa kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), imani na uchaji wa mtu. Yule ambaye ni muumini na mwenye kumcha Allaah ndiye walii.

[1] 10:62-64

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 40-42
  • Imechapishwa: 21/08/2019