28. Kujuzu kwa walima chakula kingine mbali na nyama

26- Kujuzu kwa walima mbali na nyama

Inajuzu kufanya karamu ya ndoa kwa chakula chochote kitachokuwa chepesi ijapokuwa kutakosekana nyama kutokana na Hadiyth ya Anas (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa kati ya al-Khaybar na al-Madiynah kwa muda wa siku tatu ambazo alimwingilia Swafiyyah. Akawaalika waislamu katika karamu yake ya ndoa. Hakukuweko mikate wala nyama. Kilichokuweko ni matandiko ya ngozi yalioletwa na kutandazwa na kuwekwa juu yake tende, maziwa makavu na samli safi. Watu wakala hadi wakashiba.”[1]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (07/387) na siyaaq ni yake, Muslim (04/147) na upokezi mwingine pamoja na nyongeza ni yake, an-Nasaa´iy (02/93), al-Bayhaqiy (07/259), Ahmad (03/259) na (264) na ana upokezi mwingine ukiwa pamoja na nyongeza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 151
  • Imechapishwa: 21/03/2018