Inafaa kwa mwanamke kutumia vitu vinavyoleta hedhi kwa kutimia masharti mawili:

1- Malengo yake isiwe ni kutaka kukwepa jambo la wajibu. Kwa mfano akatumia vitu hivyo kabla ya Ramadhaan ili asifunge, asiswali na mfano wa hayo.

2- Apate idhini ya mume. Kuwa na hedhi kunamfanya kutopata starehe kikamilifu. Kwa ajili hiyo asitumie kitu chenye kuzuia haki yake pasina ridhaa yake. Na ikiwa ni mtalikiwa na akatumia dawa kama hizo, basi anaharakisha kufilisi haki ya mume ya kuweza kumrejea ikiwa ni talaka rejea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016