28- Muhammad bin Muusaa as-Swayrafiy ametuhadithia: al-Aswamm ametuhadithia: Hamdaan al-Warraaq ametuhadithia: Muusaa bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Abaan ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kutatupwa Motoni na useme:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mpaka Mola wa walimwengu aweke unyayo Wake ndani ambapo utasema: “Tosha, tosha.”[2]

[1] 50:30

[2] al-Bukhaariy (4848), Muslim (2188) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 92-93.

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 58
  • Imechapishwa: 04/02/2017