28. Dalili juu ya mkono wa Allaah 14

28- Ahmad bin Muhammad bin Abiy Bakr al-Waasitwiy, Ahmad bin ´Abdillaah bin Muhammad al-Wakiyl na Muhammad bin Sahl bin al-Fudhwayl al-Kaatib amesema: ´Umar bin Shabbah ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: Mansuur na Sulaymaan wamenihadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud ambaye amesema:

“Kuna myahudi alienda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Muhammad! Hakika Allaah (´Azza wa Jall) atazibeba mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, milima kwenye kidole, miti kwenye kidole na viumbe kidole. Halafu aseme: “Mimi ndiye mfalme.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na akasema: “Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria!”

Yahyaa amesema: “Fudhwayl bin ´Iyaadhw ameongeza kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka kwa kushangazwa na kwa ajili ya kumsadikisha.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 28/02/2018