Kuhusu ambaye ataacha kufunga kutokana na udhuru unaoondoka – kama mfano wa msafiri, mgonjwa mwenye maradhi yenye kutarajiwa kupona, mjamzito au mnyonyeshaji pindi watapochelea juu ya nafsi zao wenyewe au juu ya watoto wao, mwenye damu ya hedhi au damu ya uzazi – basi kila mmoja katika hawa inamlazimu kulipa kwa njia ya kwamba watafunga masiku mengine kwa idadi ya zile siku walizokula. Amesema (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine..”[1]

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/391)
  • Imechapishwa: 28/04/2021