28. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa nne wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema kuhusu Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ

“Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni neema Yangu Niliyokuneemesheni na timizeni ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu na Mimi [pekee] niogopeni. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha; na wala msiuze ujumbe Wangu kwa thamani ndogo na Mimi tu nicheni.” (02:40-41)

“Samaa´ah bin Mahraan amesema: “Nilimuuliza Abu ´Abdillaah kuhusiana na Kauli ya Allaah:

وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ

“Na timizeni ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu.”

Akasema: “Bi maana “Timizeni uongozi wa ´Aliy ikiwa ni faradhi kutoka kwa Allaah, hivyo nitawapa Pepo.”

Mhakiki ameelekeza katika vitabu “al-Burhaan”, “al-Bihaar” na “Ithbaat-ul-Hudaah”.

al-´Ayyaashiy amesema:

“Jaabir al-Ju´fiy amesem: “Nilimuuliza Abu Ja´faar kuhusu maana ya Qur-aan iliyojificha ya Aayah:

وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ

“Aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha.”

Bi maana fulani na fulani na marafiki zake na wale wenye kuwafuata na kuwa na dini yao. Allaah Anakusudia wao:

وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ

“… na wala msiwe wa kwanza wenye kuzikanusha.”

Bi maana wale wenye kumkanusha Aliy.

Mhakiki ameelekeza katika vitabu “al-Burhaan”, “al-Bihaar” na “al-Wasaa-il”.

Tazama ukafiri na unafiki huu katika kuifasiri Kitabu cha Allaah! Wazungumzishwaji katika Aayah hizo mbili ni na zilizo baada yake ni mayahudi, ni jambo liko wazi kama jua. Allaah Anawaamrisha waiamini Qur-aan ambayo inasadikisha Tawrat na Anawakemea kuikanusha Qur-aan na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baatwiniyyah wanazipotosha Aayah hizi tukufu kwa maslahi ya madhehebu yao ya kikafiri na wanajificha nyuma ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) na kuwatuhumu Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ukafiri, na aliye mstari wa mbele kabisa ni Abu Bakr na ´Umar.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 19/03/2017