ad-Duwaysh amesema kwamba al-Albaaniy amewatukana Wahhaabiyyah na akasema:

“Mimi nina nini kuhusu Wahhaabiyyah? Pengine mimi nawakosoa zaidi kuliko mwingine yeyote. Ndugu zangu walioko hapa wanalijua hilo.”[1]

Kisha ad-Duwaysh akasema:

“Haya ni maneno khatari. Lau tutayachunguza kwa mtazamo fulani wa Kishari´ah basi maana yake ni kwamba anajitenga mbali na Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Mambo ni hivo na kwamba amejiunga na kundi linaloifanyia uadui Da´wah hii kama vile Zayniy Dahlaan, an-Nabahaaniy na makhurafi wengine wote.”[2]

Haya ni batili kwa sababu ya mambo yafuatayo:

1- Ni wajibu kwa kila mtu kumhukumu mwanachuoni kwa yale yanayotambulika kwake. Ikitokea akazungumza kwa njia iliyopinda basi tunatakiwa kurejea kwa yale yanayotambulika kwake. Ima amemsemea uongo yule aliyemnakili au pia inawezekana vilevile mwanachuoni huyo amelenga kitu tusichokijua.

2- al-Albaaniy alikuwa anatambulika kuadhimisha Da´wah ya Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na kufuata mfumo wake wakati anapolingania katika Tawhiyd na kupambana na shirki, kulingania katika Sunnah na kupambana na Bid´ah, kulingania katika Qur-aan, Sunnah kwa ufahamu wa Salaf na kutupilia mbali yote yanayokwenda kinyume na hayo. Vitabu vyake, mahojiano yake na ruduud zake zinatolea ushahidi juu ya hilo.

3- Mtu ambaye anataka kutokomeza vitabu vyake, ruduud zake na mahojiano yake kwa sababu ya neno moja alilotamka ambalo linaweza kufahamika kwa njia nzuri, basi hiyo ni dalili ya wazi inayoonyesha mtu huyo kuwa ni wa batili na ni mtu wa matamanio.

4- Neno “Wahhaabiyyah” kwa Ahl-ul-Bid´ah linafahamika vibaya. Wanasema kwamba Wahhaabiyyah wanakataza kulitambelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba hawamswalii, wanamuua na kumpiga yule mwenye kumswalia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kadhalika. Kama kweli alisema maneno hayo, basi alicholenga ni hiyo maana ya batili kutokamana na maneno ya ´Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ´anh):

“Mna vidokezo vya kutosha kwa ajili ya kuacha uongo.”[3]

Mimi nina yakini kabisa kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) hamaanishi kutukana mfumo wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na kwamba badala yake anachotaka ni kukemea na kujitenga mbali na ufahamu mbaya wa wazushi juu ya Wahhaabiyyah.

[1] Kanda ”Rihlat-ul-´Aqabah”.

[2] at-Ta´qiyb, uk. 5

[3] Tazama ”Fath-ul-Baariy” (10/594).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 05/12/2018