Download

Kusanya viganja vyako kisha uvitemee cheche za mate na usome ndani yake:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم. قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[1]

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَق مِن شَرِّ مَا خَلَقَ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ  وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa mapambazuko, kutokamana na shari ya alivyoviumba, na kutokamana na shari ya giza linapoingia, kutokamana na shari ya wapulizao mafundoni na kutokamana na shari ya hasidi anapohusudu.”[2]

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَـٰهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa watu, mfalme wa watu, mwabudiwa wa haki wa watu, kutokamana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma, anayetia wasiwasi nyoyoni mwa watu miongoni mwa majini na watu.”[3]

kisha ufute kwavyo kiasi uwezacho katika mwili wako kwa kuanza juu ya kichwa chako, uso wako na mbele ya mwili wako.

Afanye hivo mara 3[4].

100-

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anaombea mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye yujuu kabisa, Ametukuka.”[5]

101-

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ

 ”Mtume ameamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini; wote wamemuamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Mitume Yake [nao husema] ”hatutofautishi kati ya yeyote katika ya Mitume Yake” na wakasema ”Tumesikia na tumetii, tunakuomba msamaha, Mola wetu na Kwako ndiko pa kuishilia.” Allaah haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake; itapata iliyoyachuma na ni dhidi yake iliyojichumia. Mola wetu! Usituchukulie pindi tunasahau au tunakosea. Mola wetu! Usitubebeshe mzigo kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu! Usitubebeshe tusiyoyaweza, na tusamehe, na tusamehe na turehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu, hivyo basi tunusuru dhidi ya watu makafiri.”[6]

102-

بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين

”Kwa jina lako[7], Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili Yako nitaunyanyua. Ukiizuia roho yangu, basi irehemu, na ukiirejesha, basi ihifadhi kwa yale unachowahifadhi kwayo waja Wako wema.”[8]

 103-

اللّهُـمَّ إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها. اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة

”Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye umeiumba nafsi yangu na Wewe ndiye utaifisha. Ni Kwako kufa na kuhuika kwake. Ukiipa uhai, basi ihifadhi, na ukiifisha, basi isamehe. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba hifadhi na salama.”[9]

104-

اللّهُـمَّ قِنـي عَذابَـكَ يَـوْمَ تَبْـعَثُ عِبـادَك

”Ee Allaah! Nilinde[10] na adhabu Yako siku utayowafufua waja Wako.”[11]

105-

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا

”Kwa jina lako, ee Allaah, ninakufa na ninakuwa hai.”[12]

106-

سُبْـحانَ الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu”,

mara 33.

أَلْحَمْدُ لِلَّه

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah”,

mara 33.

اللَّه أكْبَرُ

”Allaah ni mkubwa.”

mara 44[13].

107-

اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ السَّبْـعِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيلِ والفُـرْقانِ. أَعُـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِهِ. اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الآخِـرُ فَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُ فَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيءٌ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْرِ

”Ee Allaah, Mola wa mbingu saba na Mola wa ’Arshi tukufu. Mola wetu na Mola wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa na aliyeteremsha Tawraat, Injiyl na Qur-aan. Najilinda Kwako kutokamana na shari ya kila kitu; Wewe ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah! Wewe ndiye  wa Mwanzo, hakuna kitu chochote kabla Yako. Wewe ndiye wa Mwisho, hakuna kitu chochote baada Yako. Wewe ndiye Uliye juu, hakuna kitu chochote juu Yako. Wewe ndiye Uliye karibu, hakuna kitu chochote kilichofichikana Kwako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.”[14]

108-

الـحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْـعَمَنا وَسَقـانا، وَكَفـانا، وَآوانا، فَكَـمْ مِمَّـنْ لا كـافِيَ لَـهُ وَلا مُؤْوِيَ

”Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, ambaye ametulisha, akatunywesha, akatutosheleza na akatuhifadhi. Kwani ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi!”[15]

109-

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيبِ وَالشّـهادةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ نَفْسـي، وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى نَفْسـي سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم

”Ee Allaah! Mjuzi wa yaliyojificha na yenye kuonekana, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu na Mwenye kukimiliki. Nashuhudia kwamba hapana mungu wa  haki isipokuwa Wewe. Najilinda Kwako kutokamana na shari ya nafsi yangu na shari ya shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu juu ya nafsi yangu au kumletea nao muislamu.”[16]

110-

Asome Suurah ”as-Sajdah” na ”al-Mulk”[17].

111-

اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت

”Ee Allaah[18]! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, nimeyaegemeza mambo yangu Kwako, nimeuelekeza uso wangu Kwako, nimeutegemeza mgongo wangu Kwako hali ya kuwa ni mwenye kukutarajia na mwenye kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ulichokiteremsha na Nabii Wako Uliyemtuma.”[19]

[1] 112:01-04

[2] 113:01-05

[3] 114:01-06

[4] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (09/62) na Muslim (04/1723).

[5] 02:255 ”Atakayeisoma atakapokuwa usiku kitandani mwake, basi atabakia katika hifadhi ya Allaah wala hatokaribiwa na shaytwaan mpaka aamke.” al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (04/487).

[6] 02:285-286 ”Ayakayezisoma [Aayah mbili hizo usiku], basi zitamtosheleza.” al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (09/94) na Muslim (01/554).

[7] ”Atakapoamka mmoja wenu kutoka kitandani mwake kisha akarudi basi akikungute kitanda kwa shuka yake mara tatu na ataje jina la Allaah, kwani hajui kilicho kuja baada yake, kisha akiweka ubavu wake kitandani aseme… .”

[8] al-Bukhaariy (11/126) na Muslim (04/2084).

[9] Muslim (04/2083) na Ahmad kwa tamko lake (02/79).

[10] ”Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitaka kulala, basi huweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake kisha anasema… ”

[11] Abu Daawuud (04/311) na tamko ni lake. Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/143).

[12] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/113) na Muslim (04/2083).

[13] ”Atakayesema hivo wakati anapopanda kitanda chake, basi ni bora kwake kuliko mfanya kazi.” al-Bukhaariy  pamoja na al-Fath (07/71) na Muslim (04/2091).

[14] Muslim (04/2084).

[15] Muslim (04/2085).

[16] Abu Dawuud (04/317). Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/142).

[17] at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy. Tazama “Swahiy-ul-Jaamiy´” (04/255).

[18] ”Unapotaka kulala, tawadha wudhuu´ kama wa swalah kisha lalia ubavu wa kulia kisha useme… “

[19] Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aliyesema hivo:

“Akifa basi amekufa juu ya maumbile.”

al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/113) na Muslim (04/2081).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 28/04/2020