275. Ni ipi tofauti kati ya matembezi ya wanawake kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makaburi mengine?

Swali 275: Ni ipi tofauti kati ya matembezi ya wanawake kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makaburi mengine? Je, makatazo ni yenye kuenea au kunabaguliwa kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hakuna dalili inayoonyesha kuwa kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) linatoka nje ya makatazo. Kwa ajili hiyo naona kuwa matembezi ya mwanamke kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kama kuyatembelea makaburi mengine. Inamtosha mwanamke kule kumsalimia kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale anaposwali. Wakati anapomsalimia basi salamu yake inamfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) popote anapokuwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/316)
  • Imechapishwa: 29/05/2022