273. Haya si ni dalili inayoonyesha kufaa kwa wanawake kuyatembelea makaburi?

Swali 273: Muslim amepokea kupitia kwa Muhammad bin Qays ambaye amesimulia kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Ee Mtume wa Allaah! Niwaambie nini?” Akasema: “Sema:

السَّلامُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الدِّيَارِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُسْلِمِين ,و يرحم الله المستقدمين منا و المستأخرين,وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللهُ بكم لاحِقُونَ نَسْأَلُ الله لَنَا وَلَكُمْ الْعَافِية

“Amani ishuke juu yenu, watu wa nyumba za waumini na waislamu. Allaah awarehemu wale waliotangulia katika sisi na wanaokuja nyuma. Na sisi – atakapo Allaah – tutakutana na nyinyi. Namuomba Allaah atupe sisi na nyinyi afya njema.”

Je, haya si yanafahamisha na maneno yake Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Tumekatazwa kusindikiza jeneza licha ya kuwa hatukufanyiwa mkazo.”[1]

na dalili nyinginezo kufaa kwa wanawake kuyatembelea makaburi muda wa kuwa hawafanyi kitu kilichoharamishwa na Allaah? Vinginevyo ni vipi mnafasiri Hadiyth ya Muhammad bin Qays?

Jibu: Nimetaja hapo kabla hukumu juu ya jambo hili na nikaashiria Hadiyth ya ´Aaishah. Nimesema kuwa Sunnah inafahamisha kwamba ni dhambi kubwa mwanamke akitoka nyumba hali ya kukusudia kuyatembelea makaburi na kwamba hakuna neno endapo itatokea akawapitia ambapo akasimama na kuwatolea salamu. Namna hiyo Sunnah inakuwa yenye kuafikiana na kunakuwa hakuna mgongano, Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) inaingia katika hali hiyo.

Kuhusu Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa), wanazuoni wengi wanasema kinachozingatiwa ni yale aliyopokea, nayo ni:

“Tumekatazwa kusindikiza jeneza… “

maneno yake aliposema:

“… licha ya kuwa hatukufanyiwa mkazo.”

ni uelewa wake. Inawezekana hayo ndio yakawa makusudio ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pengine ikawa sio makusudio. Kusindikiza jeneza ni kitu kimoja na kuyatembelea makaburi ni kitu kingine. Kwa kuzingatia kwamba wapo wanamme katika kule kulisindikiza jeneza hivyo kuna asilimia chache ya kuwepo makatazo kwa sababu wanaweza kuzuia jambo hilo. Hilo ni tofauti na matembezi ya makaburi.

[1] al-Bukhaariy (1278) na Muslim (938).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/313-315)
  • Imechapishwa: 30/05/2022