27. Wafanyakazi walioko karibu na misikiti wanaoswali makazini mwao

Swali 27: Ni ipi hukumu ya ambaye anasikia adhaana lakini haendi msikitini pamoja na kwamba anaswali nyumbani vipindi vyote vya swalah au kwenye kitengo ambacho anafanya kazi?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Lililo la wajibu kwake ni yeye kuitikia wito. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayesikia wito na asiiendee, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”

Ameipokea ad-Daaraqutwniy, Ibn Hibbaan na al-Haakim kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

Ibn ´Abbaas aliulizwa:

“Ni upi udhuru uliokusudiw?” Akajibu kwa kusema:

“Ni khofu au maradhi.”

Kuna kipofu alimwendea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Mimi sina mtu wa kunielekeza msikitini. Je, ninpata ruhusa ya kuswali nyumbani?” Akasema: “Husikia wito?” Akajibu: “Ndio.” Akasema: “Itikia.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Ikiwa kipofu ambaye hana wa kumwongoza amenyimwa ruhusa basi wengine wana haki zaidi [ya kunyimwa ruhusa].

Ni lazima kwa muislamu kukimbilia kuziswali swalah kwa nyakati zake na kwa mkusanyiko. Ama akiwa mbali ambapo hasikii adhaana ni sawa akaswali nyumbani kwake. Akipata uzito na akauvumilia na akaswali katika mkusanyiko basi hilo ni kheri na bora kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 14/10/2019