27. Wabebaji wa bendera Badr


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamfanya Musw´ab bin ´Umayr kuongoza kikosi. Akampa bendera moja ´Aliy bin Abiy Twaalib na bendera nyingine mwanamume kutoka katika Answaar. Bendera ya Answaar ilikuwa na Sa´d bin Mu´aadh. Akamfanya Qays bin Abiy Sa´sa´ kuwa msimamizi.

 Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika karibu na Swafraa´ akamtuma Basbas bin ´Amr al-Juhaniy, ambaye ni mshirika wa Banuu  Saa´idah, na ´Adiy bin Abiyz-Zaghbaa al-Juhaniy, mshirika wa Banuun-Najjaar, kwenda Badr kupeleleza khabari za msafara.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 46
  • Imechapishwa: 27/04/2018