Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

22- Hayo ni kwa sababu Yeye juu ya kila jambo ni muweza.

MAELEZO

Hii ni sifa ya milele. Haina maana kwamba alikuwa na uwezo baada ya kuwaumba viumbe. Uwezo ni sifa ya milele. Uumbaji Wake wa viumbe umetokana na kwamba Yeye juu ya kila jambo ni muweza. Allaah ndiye ambaye amesema kwamba juu ya kila jambo ni muweza katika vilivyoko na visivyokuweko na wala hakufungamanisha uwezo wake na kitu maalum. Hakuna kimshindacho. Wala haijuzu kufungamanisha kwamba ni muweza juu ya jambo fulani. Wala haitakiwi kusema kwamba Yeye ni muweza juu ya kile anachokitaka. Hayo ni yenye kuhusiana na pale ambapo Allaah atawakusanya walimwengu wote:

وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ

“Miongoni mwa ishara Zake ni uumbaji wa mbingu na ardhi na aliowatawanya humo kati ya viumbe vinavyotembea – Naye kwa kuwakusanya atakapo ni muweza.”[1]

Hii ni hali maalum.

[1] 42:29

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 45
  • Imechapishwa: 19/09/2019