27. Tushike msimamo gani ju ya mapote na makundi kutoka nje ya nchi?

Swali  27: Ni vipi unatakiwa kuwa msimamo wetu juu ya mapote ya vijana na wanafunzi yanayoingia katika mambo ambayo yanawazuia kutafuta elimu, kuwatukana baadhi ya wanazuoni na kuwa na ushabiki juu ya wengine? Swali hili ni muhimu na limeenea kati ya wanafunzi. Una nasaha zipi juu ya hilo?

Jibu: Hapo kabla wakati ambapo watu wote wa nchi hii, vijana kwa watu wazima, walipokuwa wamefungamana na wanazuoni hali ilikuwa nzuri. Hakukuwa na fikira zenye kuwajia kutoka nje ya nchi. Hili ndio sababu ya umoja na mshikamano. Watu walikuwa wakiwaamini wanazuoni, viongozi na watu wao wenye busara. Walikuwa kundi moja tu mpaka hapo kulipokuja fikira mbalimbali na watu walipokuja kutoka nje ya nchi[1] na baadhi ya vitabu na magazeti[2] yakaanza kusomwa. Vijana wakayapokea na hapo ndipo mfarakano ukatokea. Vijana hawa ambao wamepinda kutokana na mfumo wa Salaf katika ulinganizi wameathirika kwa sababu ya fikira hizi zenye kutoka nje ya nchi.

Kuhusiana na vijana ambao bado wamebaki na mawasiliano na wanazuoni wao na hawakuathirika na fikira hizi zenye kutoka nje ya nchi, hali zao ni nzuri kama wahenga wao wema waliotangulia – na himdi zote njema anastahiki kupewa Allaah[3].

[1] Mfano wa hawa ni al-Ikhwaan al-Muslimuun ambao fitina yao imeenea. Wanachukulia wepesi ´Aqiydah na wamepinda katika mfumo wa Salaf. Mfano mwingine ni Jamaa´at-ut-Tabliygh na wengineo.

[2] Mfano wa hawa ni vitabu vya al-Ikhwaan al-Muslimuun na magazeti ya Qutbiyyah kwa jina “as-Sunnah” lenye kuchanga sumu na asali.

[3] Ni Ahl-ul-Athar na Salafiyyuun ndio wenye kushikamana na Sunnah. Kutokana na ujinga wao wa Sunnah wakinzani wao ndio huwatuhumu kuwa wana misimamo mikali, vibaraka na ni wenye kujikombakomba. Hakuna cha kushangaza. Salaf walituhumiwa vibaya zaidi kuliko hivi kama “Hashwiyyah” na “Mujassimah”. Ni moja katika sifa za Ahl-ul-Bid´ah ambao huwaponda Ahl-ul-Athar.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 71-75
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy