27. Tawhiyd imesimama juu ya dalili za wazi tofauti na shirki

Kwa haya tunapata kuona kuwa washirikina hawana dalili yoyote ya sawa inayosapoti shirki waliyomo. Bali wao ni kama Allaah (Ta´ala) alivosema:

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ

“Yeyote yule anayeomba du’aa badala ya Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo.”[1]

Mambo yakishakuwa hivi kwamba shirki haikusimama juu ya hoja na dalili, basi tutambue kuwa Tawhiyd imesimama juu ya dalili za kukata kabisa na hoja za wazi:

أَفِي اللَّـهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

 “Je, kuna shaka kuhusiana na Allaah, mwanzilishi wa mbingu na ardhi.”[2]

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖفَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

”Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu ili mche. Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”[3]

[1] 23:117

[2] 14:10

[3] 02:21-22

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 43
  • Imechapishwa: 03/04/2019