27. Mwenye busara kuwa na adui kwa watu


1- Mwenye busara anatakiwa kutambua ya kwamba yule anayempenda hamhusudu na yule asiyemhusudu hawi adui yake. Kwa ajili hiyo anatakiwa kuwa mwangalifu zaidi na yule adui aliyefichikana kuliko alivyo adui na yule adui wa wazi.

2- Lililo salama zaidi kwa aliye na busara ni yeye kujitenga mbali na aina zote za adui kuliko kuziingia.

3- al-A´war ameeleza kuwa Ismaa´iyl amesema:

“Usinunue uadui wa mtu kwa mapenzi ya watu 1000.”

4- Haitakikani kwa mwenye busara kulipiza ubaya mfano wake. Haifai kwake kufanya kumlaani na kumtukana adui wake ndio silaha yake. Msaada mzuri dhidi ya adui ni kurekebisha yale mapungufu na kuficha yale makosa ili yule adui asipate kwake njia yoyote ya kumwendea.

5- Mwenye busara anatazama ni wapi pa kuweka mguu wake kabla ya kupiga hatua. Baada ya hapo anaenda karibu kidogo na adui wake. Haendi karibu naye sana ili asije kumparamia. Mwenye busara hachukii midhali anaona mapenzi ndio njia pekee. Hamchukii yeyote ambaye analazimika kuishi naye na wala adui mwenye hasira na asiyesubiriwa. Hapana hakuna njia nyingine isipokuwa kumkimbia.

6- Msimamo imara kwa adui ni kutomzungumza vibaya midhali si katika nafasi ya kufanya hivo. Ushindi mkubwa dhidi ya maadui ni mtu kuwaacha wakajishughulisha wao kwa wao.

7- Ibn-us-Simaak amesema:

“Usimwogope yule unayejihadhari naye. Mwogope yule unayemwamini.”

8- Uadui baada ya urafiki ni jambo baya kabisa. Haimstahikii mwenye busara kufanya kitu kama hicho. Ikitokea akatumbukia ndani yake, basi ahakikishe suluhu ina nafasi yake.”

9- ´Abdullaah bin Hasan alisema kumwambia mwana wake Muhammad:

“Ninakutahadharisha kuwa na uadui kwa watu. Uadui haukusalimishi kutokamana na njama za wajanja wala dhambi za watenda madambi.”

10- Haimpasi mwenye busara kamwe kuwa na uadui na yeyote. Kwa kuwa uadui unaweza kumkumba njama za mjanja ambaye kamwe huwezi kujisalimisha na njama zake au matusi ya mtenda dhambi ambaye kamwe huwezi kujisalimisha na marusi yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 94-98
  • Imechapishwa: 16/02/2018