Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Ni kule kuacha kuabudu mwengine asiyekuwa Allaah katika vinavyoabudiwa vyote. Hayo ndio yanayofahamishwa na makanusho pale tunaposema “Hapana mungu wa haki”. Sambamba na hilo mtu akamwabudu Allaah, hali ya kuwa pekee yake hana mshirika. Hayo ndio yanayofahamishwa na uthibitishaji pale tunaposema “Isipokuwa Allaah”. Wengi wanaolitamka wanakwenda kinyume na muqtadha yake na hivyo utawaona wanathibitisha uungu wa viumbe vile vilivyokanushwa, makaburi, makuba, waungu wa batili, miti na mawe. Watu hawa wameitakidi kuwa eti Tawhiyd ni Bid´ah, wakamkaripia yule anayewalingania kwayo na wakamkejeli yule anayemtakasia ´ibaadah Allaah.
2- Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Muhammad ni Mtume wa Allaah”. Ni kule kumtii, kumsadikisha, kuacha yale aliyokataza, kukomeka juu ya kutendea kazi Sunnah, kujiepusha na vyenginevyo katika Bid´ah na mambo mepyamepya yaliyozuliwa na kutanguliza maneno yake mbele ya maneno ya mwengine yeyote.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 51
- Imechapishwa: 20/02/2020
Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Ni kule kuacha kuabudu mwengine asiyekuwa Allaah katika vinavyoabudiwa vyote. Hayo ndio yanayofahamishwa na makanusho pale tunaposema “Hapana mungu wa haki”. Sambamba na hilo mtu akamwabudu Allaah, hali ya kuwa pekee yake hana mshirika. Hayo ndio yanayofahamishwa na uthibitishaji pale tunaposema “Isipokuwa Allaah”. Wengi wanaolitamka wanakwenda kinyume na muqtadha yake na hivyo utawaona wanathibitisha uungu wa viumbe vile vilivyokanushwa, makaburi, makuba, waungu wa batili, miti na mawe. Watu hawa wameitakidi kuwa eti Tawhiyd ni Bid´ah, wakamkaripia yule anayewalingania kwayo na wakamkejeli yule anayemtakasia ´ibaadah Allaah.
2- Muqtadha ya kushuhudia ya kwamba “Muhammad ni Mtume wa Allaah”. Ni kule kumtii, kumsadikisha, kuacha yale aliyokataza, kukomeka juu ya kutendea kazi Sunnah, kujiepusha na vyenginevyo katika Bid´ah na mambo mepyamepya yaliyozuliwa na kutanguliza maneno yake mbele ya maneno ya mwengine yeyote.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 51
Imechapishwa: 20/02/2020
https://firqatunnajia.com/27-muqtadha-za-shahaadah-mbili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)