27. Msingi wa tisa: Kuwatenga na kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah

9- Kuwatenga na kutahadharisha watu kutokamana na Ahl-ul-Bid´ah

Salaf wameafikiana juu ya kuwaweka mbali Ahl-ul-Bid´ah na kutahadharisha nao. Hayo yamesimuliwa na Abu Ya´laa na wahakiki wengineo.

Miongoni mwa mambo ambayo ni muhimu kuzindua katika suala hili ni kwamba wazushi wanajificha kwa vazi la Sunnah, wanajificha nyuma ya jina lake na wakati huohuo wamezama ndani ya Bid´ah. Anayatambua hayo kila yule mwenye kuwaangalia kwa ukaribu na akayaona yale mambo ya uvyamavyama, mipango, majaribio ya kufanya uasi kwa watawala wa waislamu, kuvunja viapo vya utiifu na mengineyo waliyojificha nyuma yake.

Mtindo huu wa Ahl-ul-Bid´ah hii leo ndio mtindo uleule wa Ahl-ul-Bid´ah hapo kale. Hivi ndivo zinavoenea Bid´ah zao na kukita ndani ya mioyo. Ibn Battwah (Rahimahu Allaah) amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Mufadhdhwal bin Muhalhal – ambaye ni mmoja katika waaminifu, wafanya ´ibaadah sana na watu wa Sunnah – kwamba amesema:

“Ingekuwa unapokaa mbele ya mzushi anakuzungumzia Bid´ah zake, basi ungemtahadharisha na kukimbia mbali naye. Lakini anavofanya ni kwamba mwanzoni mwa kikao chake anakuzungumzisha mazungumzo ya Sunnah kisha baadaye ndio anapenyeza Bid´ah zake na pengine wakati huo zimekwishalazimiana na moyo wako. Hebu nambie ni lini zitatoka nje ya moyo wako?”[1]

Kutokana na sababu hii yenye kuzingatiwa ambayo ni kuingia kwa Bid´ah ndani ya moyo na mtu asije kufungamana nayo ndio maana Salaf (Rahimahumu Allaah) walikuwa hawasikilizi maneno ya wazushi. Walikuwa wakitilia pupa kwelikweli kujitenga mbali na yale maeneo yote ambayo wazushi wanazungumza.

[1] ”al-Ibaanah” (02/444).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 12/11/2020