27. Mke asifunge isipokuwa kwa idhini ya mume

Miongoni mwa haki za mume juu ya mke wake ni yeye kutofunga Swawm ya Sunnah wakati mume wake yupo bila ya idhini yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke kufunga kwa kuwepo mume wake isipokuwa kwa idhini yake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (5195) na Muslim.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 41
  • Imechapishwa: 24/03/2017