27. Matunda ya elimu: kuenea kwa faida za msomi

7- Katika matunda ya elimu ni kuenea kwa faida sahihi. Mwanafunzi faida zake zinaenea na zinakuwa ni sahihi. Sio kila faida yenye kuenea inakuwa sahihi. Manufaa ya mtu yanaweza kuenea na akadhania kuwa ni yenye kunufaisha, lakini yakawa ni kinyume chake. Manufaa hayawi sahihi isipokuwa ikiwa yanatokamana na elimu. Mwanafunzi elimu yake ni yenye kuenea. Kwa ajili hii wanachuoni wamesema:

“Miongoni mwa siri za kufadhilishwa mwanachuoni juu ya mfanya ´ibaadah ni kuwa manufaa ya mwanachuoni ni yenye kuenea wakati manufaa ya mfanya ´ibaadah yamekomeka na yeye mwenyewe.”

Mwanachuoni manufaa yake ni yenye kuenea ambapo anafundisha na anaeneza kheri, kitendo ambacho kina ujira mkubwa. Allaah (´Azza wa Jall) anaunufaisha Ummah kupitia yeye, Allaah anazihuisha nyoyo kupitia yeye na anawaokoa watu kutoka kwenye ujinga.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016