27. Kuonja chakula mchana wa Ramadhaan


Swali 27: Ni upi hukumu ya kuonja chakula mchana wa Ramadhaan ilihali mwanamke amefunga?

Jibu: Hukumu yake ni kwamba hakuna neno kwa sababu haja imepelekea kufanya hivo. Lakini ateme kile alichoonja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 23
  • Imechapishwa: 26/07/2021