Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Inatakiwa kuamini Mizani siku ya Qiyaamah. Hadiyth inasema:

“Mja atapimwa siku ya Qiyaamah na hatokuwa na uzito sawa na bawa la mbu.”[1]

Matendo ya waja yatapimwa, kama ilivyotaFjwa kwenye mapokezi. Yanatakiwa kuaminiwa na kuthibitishwa. Mwenye kurudisha hilo anatakiwa kupuuzwa na asijadiliwe.”

MAELEZO

Ataletwa mtu mnene siku ya Qiyaamah. Mbele ya Allaah hatokuwa na uzito sawa na bawa la mbu. Hii ni dalili yenye kuonesha kuwa watu watapimwa. Imethibiti jinsi Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) alivyopanda juu ya mti na wakaona muundi wake mwembamba. Wakashangazwa nao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Je, mnashangazwa na wembamba wa miundi wake? Itakuwa na uzito kwenye mizani zaidi ya mlima wa Uhud.”[2]

Hii ni dalili yenye kuonesha kuwa watu watapimwa. Kuhusiana na matendo, hakuna tofauti yoyote juu ya kwamba yatapimwa.

Mu´tazilah, Jahmiyyah na watu wapotevu wengine wakapinga Mizani. Wanakanusha mizani ya kikweli. Hivi ndivyo wanavyosema Mu´tazilah, Jahmiyyah na wapotevu wengine. Wanapinga mizani.

[1] al-Bukhaariy (4729) na Muslim (2785).

[2] Ahmad (3991). Ahmad Shaakir amesema: ”Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.” al-Albaaniy ameitaja katika ”as-Silsilah as-Sahiyhah” (2750) na (3192).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 391
  • Imechapishwa: 26/08/2017