27. Kuamini kwamba wapwekeshaji watenda madhambi watatoka Motoni

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“… na watu wataotoka Motoni baada ya kuungua na kuwa majivu. Watapelekwa kwenye mto karibu na mlango wa Pepo, kama ilivyopokelewa katika upokezi. Yatapitika namna anavyotaka Allaah na kama anavyotaka Allaah. Si vyengine isipokuwa inahusiana na kuamini na kusadikisha hilo.”

MAELEZO

Hii ni dalili inayofahamisha kwamba wale waislamu watenda madhambi watakufa ndani ya Moto. Kuhusu wale makafiri hawatokufa ndani yake na wala hawatokuwa na uhai.

Mto wa uhai uko ndani ya mlango wa Pepo. Watawekwa ndani yake. Baada ya hapo wataanza kukuwa kama inavyokua mbegu iliyobebwa na mafuriko[1][2].

Khawaarij na Mu´tazilah wamekanusha uombezi, kwa sababu wanaona kuwa waislamu watenda madhambi makubwa watadumishwa Motoni milele.

[1] Ibn-ul-Athiyr amesema: ”Kama vile povu na udongo.” (an-Nihaayah (1/442)).

[2] al-Bukhaariy (6560) na Muslim (184).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 123-124
  • Imechapishwa: 24/04/2019