27. Du´aa wakati wa upepo


126- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Upepo ni katika Rahmah ya Allaah. Unakuja kwa Rahmah na unakuja kwa adhabu. Mnapouona msiutukane. Muombeni Allaah kheri yake na muombeni kinga kutokana na shari yake.”

127- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunapokuwa upepo alikuwa akisema:

اللَّهُمَّ إِني أَسْأَلك خيرها وخيرَ مَا فِيها وخيرَ ما أُرْسِلَتْ بِهِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّها وَشر مَا فِيهَا وشَرَّ ما أُرسلت به

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri yake, kheri ya kilicho ndani yake na kheri ya uliyoituma ndani yake. Na najikinga Kwako kutokana na shari yake, shari iliyomo ndani yake na shari iliyotumwa nao.”

128- Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anaona kutawanyika kwa mawingu katika upeo wa macho anaacha anachokifanya hata kama ni Du´aa na kusema:

اللهُمَّ إِنِي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا

“Ee Allaah! Ninakuomba kinga dhidi ya shari yake.”

Kunapoanza kunyesha anasema:

اللَّهُمَّ صيِّباً هَنيئاً

“Ee Allaah! [Ijaalie iwe ni] yenye kumiminika yenye kunufaisha”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 21/03/2017