27- Hamzah bin Muhammad al-Ja´fariy ametuhadithia: ´Abdul-Wahhaab bin al-Hasan ametuhadithia Dameski: Abuu Hawdhw ametuhadithia: Ibn Mathruud ametuhadithia: Ibn-ul-Qaasim ametuhadithia, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Abuuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anawacheka watu wawili. Mmoja wao kamuua mwengine na wote wawili wanaingia Peponi.”[1]

az-Zuhriy na Ibn ´Uyaynah wamesema:

“Mshirikina amemuua muislamu, kisha akasilimu halafu akafa.”

[1] Ahmad (27464), al-Bukhaariy (2826), Muslim (1890), Ibn Maajah (191) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 234.

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 57
  • Imechapishwa: 03/02/2017