27 Dalili ya ishirini na tano kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


25- ´Abdullaah bin Mansuur alisomewa na mimi huku nasikiza: Abul-Husayn al-Mubaarak bin ´Abdil-Jabbaar amekukhabarisheni: Muhammad bin ´Abdil-Waahid ametuhadithia: Abu Bakr bin Shaadhaan ametuhadithia: Abu ´Abdillaah bin al-Mughallas ametuhadithia: Sa´iyd bin Yahyaa al-Umawiy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia kutoka kwa Ma´bad bin Ka´b bin Maalik ambaye amesema:

“Baada ya Sa´d bin Mu´aadh kuwahukumu Banuu Quraydhwah Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia: “Umewahukumu kwa hukumu ambayo amehukumu kwayo Allaah juu ya mbingu ya saba.”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa adh-Dhahabiy katika ”al-´Uluww”, uk. 32

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 108
  • Imechapishwa: 07/06/2018