27. Dalili juu ya mkono wa Allaah 13

27- al-Qaadhwiy al-Husayn bin Ismaa´iyl, Muhammad bin Ibraahiym bin Hafsw bin Shahiyn, Ismaa´iyl bin ´Ayyaash al-Warraaq, Muhammad bin Makhlad na wengineo wametuhadithia: Muhammad bin al-Waliyd al-Baswriy ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan: Mansuur na Sulaymaan wamenihadithia, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa´Abiydah, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

“Kuna myahudi alienda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Muhammad! Hakika Allaah (´Azza wa Jall) atazibeba mbingu kwenye kidole, ardhi kwenye kidole, milima kwenye kidole, miti na viumbe kidole. Halafu aseme: “Mimi ndiye mfalme.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana na akasema: “Hawakumkadiria Allaah vile inavyostahiki kumkadiria!”

Yahyaa amesema: “Fudhwayl bin ´Iyaadhw ameongeza kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa ´Abdullaah aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka kwa kushangazwa na kwa ajili ya kumsadikisha.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 28/02/2018