27. Anayefunga swawm ya Sunnah na akamjamii mkewe kwa kusahau aendelee kufunga au inamlazimu kitu?


Swali 27: Mtu mwenye kufunga swawm ya Sunnah na akamjamii mke wake kwa kusahau aendelee kufunga au inamlazimu kitu?

Jibu: Kitendo cha kusahau inapokuja katika jamii kiko mbali. Kwa sababu jimaa ni jambo la kushirikiana baina ya mwanaume na mwanamke. Mmoja katika wanandoa akisahau mwingine atamkumbusha. Jimaa inahitajia kufunga milango na mambo mengine yanayopingana na kusahau.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 12/06/2017