27. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa tatu wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema kuhusu Kauli ya Allaah (Ta´ala):

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Pale ambapo uongofu utakufikieni kutoka kwangu, yeyote atakayefuata uongofu Wangu hakutakuwa na khofu juu yao wala hawatahuzunika.” (02:38)

“Jaabir amesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far kuhusu maana ya Qur-aan iliyojificha ya Aayah:

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Pale ambapo uongofu utakufikieni kutoka kwangu, yeyote atakayefuata uongofu Wangu hakutakuwa na khofu juu yao wala hawatahuzunika.” (02:38)

Akasema: “´Aliy ndio uongofu. Allaah Amesema kuhusu yeye:

فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

“Yeyote atakayefuata uongofu Wangu hakutakuwa na khofu juu yao wala hawatahuzunika.”[1]

Raafidhwah wanacholenga ni kwamba wao ndio wafuasi wa ´Aliy na hivyo hawatokuwa na khofu wala hawatohuzunika. Wengine wote wasiokuwa Raafidhwah, na khaswa Maswahabah, mafikio yao ni Motoni. Tazama upotoshaji na mchezo huu. Wanaozungumzishwa hapa ni wana wa Aadam (´alayhis-Salaam) mpaka siku ya Qiyaamah. Uongofu ni yale yaliyokuja na Mitume ikiwa ni pamoja na Qur-aan. Baatwiniyyah wamegeuza Aayah hii katika maana ya ufinyu kwa kumzulia Allaah uongo.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/41-42).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 59
  • Imechapishwa: 19/03/2017