Ama kumtuhumu kwamba al-Albaaniy alikuwa Hizbiy, anaafikiana pamoja na Hizbiyyuun au kwamba anakubaliana na mambo ya vyamavyama ni kumzulia pia uongo. Yeye mwenyewe amesema:

“Hasan al-Bannaa hakuwa Salafiy inapokuja katika ´Aqiydah wala mfumo.”[1]

Amemkosoa katika nukta nyingi baada ya kusema yafuatayo:

“Hasan al-Bannaa anatakiwa kushukuriwa kwa njia ya kwamba amewatoa vijana waliopotea kutoka kwenye migahawa, sehemu za pumbao na sinema na kwamba amewatoa kutoka katika baadhi ya viza na kuwaingiza katika baadhi ya nuru.”

Pamoja na kwamba Hasan al-Bannaa amekubaliana nao katika shirki kubwa. Ni nuru ipi ambayo amewaingiza ndani yake? Huenda Shaykh hakujua kuwa mtu huyu alitumbukia katika shirki kubwa na Wahdat-ul-Wujuud. Kwa hali yoyote, alipambana na mambo ya vyamavyama vibaya sana. Amesema tena:

“Viapo vya utiifu wanavyopewa manhaj hizi vinasababisha mpasuko mkubwa. Yule mwenye kula kiapo cha utiifu juu ya manhaj fulani basi ni lazima achukue manhaj zengine zote.”

[1] 1418/07/22

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 52
  • Imechapishwa: 03/04/2019