Swali 27: Je, kusema “Subhaan Allaah” kwa kunyanyua sauti siku ya ijumaa kabla ya swalah kwa saa moja au zaidi ni kitendo cha Sunnah au Bid´ah[1]?

Jibu: Hapana shaka kuwa kitendo hicho ni Bid´ah. Kwa sababu haikutufikia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake kwamba walifanya hivo. Kheri yote inapatikana kwa kuwafuata.

Kuhusu ambaye atasabihi kati yake yeye na nafsi yake hapana vibaya. Bali kufanya hivo kuna kheri kubwa na thawabu nyingi. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Maneno yanayopendeza zaidi kwa Allaah ni manne; Subhaan Allaah, Alhamdulillaah, Laa ilaaha illa Allaah na Allaahu Akbar.”[2]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Maneno mawili, mepesi kwenye ulimi, mazito kwenye mizani, yanayopendeza kwa Mwingi wa huruma:

سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake na Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu Aliye mtukufu.”[3]

Zipo Hadiyth nyingi juu ya fadhilah aina mbalimbali ya Dhikr.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/413-414).

[2] Muslim (2137) na Ahmad (19601).

[3] Imaam Ahmad (7127), al-Bukhaariy (6682) na Muslim (2694).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 67
  • Imechapishwa: 30/11/2021