26. Wajibu kwa bwanaharusi kufanya karamu


24- Uwajibu wa walima

Ni kwa mwanaume kufanya karamu ya harusi baada ya maingiliano. Hili ni kutokana na maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwamrisha ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf – kama itavyokuja – na kutokana na Hadiyth ya Buraydah bin al-Haswiyb aliyesimulia: ”Wakati ´Aliy alipomposa Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anh) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Ni lazima harusi… “

Katika upokezi mwingine:

“… wanaharusi wafanyiwe karamu.”[1]

Ndipo Sa´d akasema: “Mimi nitajitolea kondoo.” Mwengine akasema: “Mimi nitajitolea kadhaa na kadhaa katika mahindi.”

Katika upokezi mwingine:

“Kundi la Answaar wakakusanya mahindi mengi.”

[1] Ameipokea Ahmad (05/359), at-Twabaraaniy (01/112/1), at-Twahaawiy katik “al-Mushkil” (04/144-145), Ibn ´Asaakir (88/12/02) na (02/124/15). Utimilifu wake utakuja huko mbele katika kurasa ya 173-174. Mlolongo wa wapokezi wake ni kama alivyosema al-Haafidhw katika “al-Fath”:

“Hauna neno.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 142-144
  • Imechapishwa: 19/03/2018