4- Uharamu wa kufunga siku ya shaka ambayo ni ile siku ya tarehe thelathini Sha´baan ikiwa mbinguni juu kuna vikwazo vya kuona mwezi mwandamo. Mbinguni juu kukiwa kweupe basi hapo hakuna shaka yoyote. Dalili ya uharamu ni Hadiyth ya ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Yule mwenye kufunga siku ambayo ana shaka kwayo basi amemuasi Abul-Qaasim.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asiitangulizie mmoja wenu Ramadhaan kwa kufunga siku moja au siku mbili; isipokuwa ikiwa ni mtu aliyezowea kufunga swawm yake basi aendelee kuifunga.”

Maana yake ni kwamba asiitangulizie yeyote Ramadhaan kwa kufunga siku moja kwa lengo la kujichunga na kufanya lililo salama zaidi. Kwani swawm ya Ramadhaan imefungamana na kuonekana kwa mwezi mwandamo. Kwa hiyo hakuna haja ya kujikakama.

Kuhusu yule ambaye alikuwa na swawm amezowea kufunga hakuna ubaya kwake. Kwa sababu kufanya hivo sio katika kujiandaa kwa ajili ya Ramadhaan. Swawm zengine pia zilizovuliwa ni swawm za kulipa na swawm za nadhiri kutokana na ulazima wake.

5- Ni haramu kufunga zile siku mbili za ´iyd mbili. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufunga siku ya [´Iyd] al-Fitwr na [siku ya] kuchinja.”

Pia ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufunga siku mbili hizi; siku ya kufungua kwenu kutokamana na funga yenu na siku nyingine ambayo mnakula kutokana na vichinjwa vyenu.”

[1] Ameiweka taaliki al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” kwa njia ya kukata. al-Fath (04/143). Pia at-Tirmidhiy ameipokea kwa cheni ilioungana (689) na akasema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

al-Albaaniy ameisahihisha katika ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (553).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 165-166
  • Imechapishwa: 17/05/2020