1- Kukubali ujumbe wake na kuuamini ndani ya moyo.

2- Kuyatamka na kuyakubali kwa nje kwenye mdomo.

3-  Kumfuata kwa njia ya kwamba mtu afanyie kazi ile haki aliyokuja nayo na ajiepushe na ile batili aliyokataza.

4- Kumsadikisha mambo yaliyojificha aliyokhabarisha yaliyopita na yatayokuja huko mbele.

5- Mtu ampende zaidi ya anavyoipenda nafsi, mali, watoto, wazazi wake na watu wengine wote.

6- Kuyatanguliza maneno yake mbele ya maneno ya yeyote na kutendea kazi Sunnah zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 19/02/2020