145- Muslim amepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati mtu alipokuwa katika ardhi ya wazi alisikia sauti kutoka kwenye wingu ikisema: “Imwagilie maji ardhi ya fulani na fulani”, ambapo tahamaki mawingu yakaanza kutikisika na kuteremsha maji yake ardhini na maji yote yakaingia kwenye mfereji. Akayafuata yale maji na akakutana na mtu amesimama kwenye bustani yake na akilinda maji. Akamwambia: “Ee mja wa Allaah! Unaitwa nani?” Akasema jina lake jina ambalo alilisikia kwenye mawingu na akamuuliza: “Ee mja wa Allaah! Kwa nini waniuliza jina langu?” Akajibu: “Nimesikia sauti kutoka kwenye wingu lililokuja na maji haya likitaja jina la mwenye bustani. Unafanya nini kwayo [bustani hiyo]?” Akajibu: “Mimi huangalia yale yenye kutoka humo na kutoa swadaqah theluthi yake, mimi na familia yangu tunakula theluthi yake na huacha theluthi yake.”[1]

146- Katika upokezi mwingine imekuja:

“Huwapa theluthi yake masikini.”

147- Wanachuoni wetu wamesema:

“Ilipokuwa hakuna namna ya kutochukua sehemu ya vitu vya dunia, basi kuna mpaka na mpaka huo ni riziki.”

148- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Binaadamu hajapatapo kujaza chombo chenye shari kama tumbo. Inatosha kwa mwanaadamu kuchukua kipande kidogo ili kuunyoosha mgongo wake. Endapo hakuna budi [achukue zaidi] basi theluthi iende katika chakula chake, theluthi katika kinywaji chake na theluthi kwa ajili ya kupumua.”[2]

at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

149- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Godoro moja la mwanaume, godoro lingine la familia, godoro lingine la wageni na godoro lingine la shaytwaan.”[3]

150- Wanachuoni wanasema kuwa hamu ya mja inatakiwa kufungamana na haya na anatakiwa kujitahidi yale yaliyopangwa mpaka Allaah aweze kumpa zaidi. Lakini hata hivyo haifai kwake akapakana mafuta katika dini na akaingizwa katika batili kwa ajili ya kuifikia.

[1] Muslim (2984) na Ahmad (2/296).

[2] at-Tirmidhiy (2486).

[3] Muslim (14/59).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 18/03/2017