Swali 26: Katika baadhi ya misikiti katika sehemu kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu kunasomwa Aayah za Qur-aan tukufu kupitia kipaza sauti na hayo yanafanyika kabla ya swalah ya ijumaa. Ni ipi hukumu[1]?

Jibu: Hatutambui msingi wa hilo kutoka katika Qur-aan, Sunnah, matendo ya Maswahabah wala matendo ya wema waliotangulia (Radhiya Allaahu ´anhum). Jambo hilo linazingatiwa – kwa mujibu wa vile lilivyotajwa – ni miongoni mwa mambo yaliyozuliwa ambayo inatakiwa kuyaacha. Kwa sababu ni jambo lililozuliwa. Jengine ni kwa sababu linaweza kuwashughulisha waswaliji na wasomaji kutokamana na swalah na kisomo chao.  Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/413).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 30/11/2021