26. Ni kweli kwamba Shyakh Rabiy´ anawaponda wanachuoni?


Swali 26: Unajua nini kuhusiana na ukaribu wako kwa wanachuoni wa al-Madiynah kwa sura ya jumla na khaswa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy? Vijana wengi wanasema kuwa Shaykh Rabiy´ anawatukana wanachuoni. Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Huku ni kupindua uhakika wa mambo. Shaykh Rabiy´ hakumtukana mwanachuoni yeyote aliyenyooka ambaye ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Amemponda yule ambaye ameanza kitu katika Bid´ah na mfano wa hayo. Shaykh Rabiy´ ni katika Ahl-us-Sunnah na wengine al-Madiynah wanaofuata mfumo wake. Wote ni Ahl-us-Sunnah. Hawaitwi kuwa ni Ahl-ul-Bid´ah. Hizbiyyuun ndio wenye kuwaita hivo ambao wanataka kupindua uhakika wa mambo. Wanakuja watu wajinga ambao viongozi wao wanawapachika maneno wanayodhania kuwa ni haki ilihali ni batili.

Ni wajibu kwa wanafunzi kushikamana na haki. Ambaye anatetea ´Aqiydah ya Tawhiyd na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah haisemwi kuwa anawatukana wanachuoni. Kwani mtu huyu anazindua makosa wanayofanya watu  hawa ambao amewazungumzia kwa ubaya kwa kuzingatia ya kwamba ni wazushi wa asli au wanawasapoti watu wazushi. Malengo yake akataka kuwazindua ili kuunasihi Ummah. Ikiwa anafanya hivo kwa lengo la kuunasihi Ummah haisemwi kuwa anawatukana wanachuoni. Maneno haya sio ya kweli. Yanasemwa na Hizbiyyuun. Lengo lao wanataka watu wa al-Madiynah na wanafunzi wawachukie na kuwakimbia Salafiyyuun. Hizi ni hila za Hizbiyyuun. Wanachotaka ni wapotee pamoja nao.

Wanachuoni wa al-Madiynah wote akiwemo Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy, Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy, Shaykh ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy, Shaykh Muhammad bin Rabiy´, Shaykh Muhammad bin Haadiy na wengine wenye kufuata mfumo wao wote ni Ahl-us-Sunnah. Inatakiwa kuchukua maneno yao, kusikiliza mikanda na mihadhara yao. Kadhalika Swaalih bin ´Abuud, ´Abdur-Razzaaq al-´Abbaad na wengineo walio pamoja nao.

Muhimu ni kuwa watu hawa wako juu ya haki na juu ya Sunnah na juu ya njia iliyonyooka. Ni wajibu kwa wanafunzi kusikiliza mikanda na mihadhara yao. Kadhalika wahudhurie darsa zao ili wafaidike na utata uwaondoke.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017